Polisi Wamkama Mwanaume Aliyechapa Mwanaye Mpaka Kufa Kisa Kukojoa Kitandani

akamatwa

Polisi wa Kituo cha polisi cha Webuye katika kaunti ya Bungoma huko nchini Kenya wamemtia mbaroni mwanaume mmoja baada ya kumchapa mwanawe wa kambo hadi kufa baada ya kukojoa kitandani.

Mashahidi walioongea na wanahabari walisema kuwa mwanaume huyo alimchapa mwanawe kichapo cha mbwa Alhamisi asubuhi na mapema na kumuacha kando ya barabara.

Majeraha aliyoyapata mtoto huyo yalimpelekea kufikia kifo chake.Wakaazi wa eneo hilo walimtia  mwanaume huyo  adhabu kwa kitendo hicho lakini polisi waliwasili mapema kabla ya kuchapwa.

Polisi wamemshika mshukiwa huyo wakati uchunguzi wa kisa hicho unapoendelea, na mwili wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuifadhia maiti cha Webuye.

dj celebu app
 
DJ Celebu
Author: DJ Celebu

Leave a Reply