Australia yataka masoko ya wanyamapori kufungwa

Australia imetoa wito kwa kundi la mataifa yanayoinukia ya G20 kukomesha masoko yanayouza wanyamapori kutokana na kitisho chake kwa afya ya binadamu na bidhaa za kilimo.

Waziri wa Kilimo wa Australia David Littleproud amesema amewambia maafisa wa serikali za kundi la G20 kuunga mkono wazo la kuyafunga masoko yote yanayouza wanyamapori kama chakula.

Wito kama huo umetolewa pia na maafisa wa Marekani waliohimiza kufungwa kwa masoko yote yanayouza nyama mbichi za porini barani Asia.

Hatua hiyo ya Australia inaweza kuchochea kudorora kwa mahusiano yake na China ambayo inadhaniwa kuwa soko la wanyama pori katika mji wa Wuhan ndiyo lilikuwa chanzo cha kuzuka kwa virusi vya corona.

Ingawa waziri Littleproud hakuitaja China moja kwa moja lakini matamshi yake yanafuatia shinikizo la Australia la kutaka jumuiya ya kimataifa ianzishe uchunguzi kuhusu chanzo na jinsi China ilivyoshughulikia mlipuko wa virusi vya corona.

About Celebu 5988 Articles
Number 1 Online Kenya/East Africa Music Distributions and Promotion, All Rights Reserved. On DJ Celebu website we offer you some DJ Mixtapes, Gengetone, RnB, Hip Hop, Reggae, Gospel, Bongo Flava, Taarab, Asili, Mp3 Audio Downloads, Mp4 Videos Downloads.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*