Swahili News

Jaji wa Brazil aamuru uchunguzi kuhusu shutuma dhidi ya Bolsonaro

on

[ad_1]

Jaji wa mahakama kuu nchini Brazil ameamuru uchunguzi kuhusiana na shutuma zilizotolewa na waziri wa zamani wa sheria na usalama, Sergio Moro, kuwa Rais Jair Bolsonaro alitaka kuingilia uchunguzi wa polisi.

Katika uamuzi wake wa hapo jana, uliopatikana na shirika la habari la AFP, Jaji Celso de Mello ameipa polisi ya nchi hiyo siku 60 kumhoji Moro juu ya madai yake hayo dhidi ya rais wa nchi hiyo. Uchunguzi wake ambao utakabidhiwa kwa mwanasheria mkuu, unaweza kusababisha ama ombi la kesi ya kisiasa dhidi ya Bolsonaro ama kushitakiwa Moro kwa kutoa ushahidi wa uongo.

Kwa mujibu wa jaji huyo, madai ya uhalifu unaonekana kuwa na uhusiano wa karibu na madaraka ya rais, na kwa hiyo yanahitaji uchunguzi dhidi ya kiongozi huyo.

Moro, jaji wa zamani wa kupambana na rushwa, alijiuzulu siku ya Ijumaa baada ya kupambana na Bolsonaro kuhusiana na kufukuzwa kwa mkuu wa polisi, akimshutumu rais kwa kuingilia masuala ya kisiasa.

[ad_2]

About Richard Wanyonyi

Richard Wanyonyi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *