Kamati ya usalama yahimiza usimamizi wa sheria kuikabili corona

Na Thabit Madai,Zanzibar.

KAMATI ya ulinzi na usalama ya kitaifa imeutaka uongozi wa mkoa wa mjini magharibi unguja kusimamia maswala ya usafi wa mazingira na kusimamia kikamilifu sheria ili kukabiliana na mripuko wa maradhi.

Kamati hiyo inayoongozwa na Bregedia Fadhil Omar Nondo imetoa maelekezo hayo katika kikao cha pamoja kati ya kamati hiyo, uongozi wa mkoa na mabaraza ya manispaa kilichofanyika katika ofisi za mkoa huo Vuga.

Kikao hicho ambacho kilitanguliwa na ziara ya kamati hiyo katika maeneo mbali mbali yakiwemo ya masoko na bandari ya Malindi iliyolenga kubaini utekelezaji wa maagizo ya serikali katika vita dhidi ya maradhi ya covid 19.

Kamati hiyo imeeleza kuwa katika ziara hiyo imebaini changamoto kadhaa ikiwemo ya usimamizi wa sheria kwa maagizo na maelekezo yanayotolewa na serikali jambo ambalo linapaswa kuzingatiwa na mamlaka zote mkoani humo.

“Katika maeneo tuliyotembelea hasa masokoni bado maelekezo ya serikali na wataalamu wa afya yakiwemo ya kuepuka mikusanyiko yanapuuzwa na hapa kinachokosekana ni usimamizi madhubuti wa sheria tu,” alieleza Katibu wa kamati hiyo.

Aidha kamati hiyo imepongeza hatua zinazochukuliwa na viongozi hao pamoja na taasisi zinazohusika na usafiri wa baharini katika mapambano ya maradhi yazaidi kuwekwa katika maeneo mengine.

“hali tuliyoikuta bandarini inaonesha mabadiliko sasa kinachotakiwa tuendelee kuwaelimisha watu wetu na ikibidi tutumie sheria ili kuushinda ugonjwa huu jambo ambalo limo ndani wa mamlaka yenu,” alisema.Wakiwa katika bandari ya malindi, mkurugenzi wa ulinzi na udhibiti katika Mamlaka ya usafiri baharini Msilimiwa Idi Juma aliiambia kamati hiyo kuwa pamoja na mambo mengine wamevitaka vyombo vya usafiri baharini kupunguza idadi ya abiria wao ili kupunguza msongamano.

Alisema wamekubaliana na vyomvo hivyo kupunguza idadi hiyo kwa asilimia hamsini sambamba na kuzingatia umuhimu wa kupeana nafasi katika maeneo ya ukaaji ndani ya vyombo vyao.

“Kwa mfano Kilimanjaro 7 ina uwezo wa kuchukua abiria 510 lakini katika safari hii imechukua abiria 170 pekee lakini pia tumewataka kuzingatia kanuni za afya ikiwemo kuwapatia abira wao vikinga uso (maski),” alieleza Msilimiwa.

Akizungumza hatua wanazochukua katika ziara hiyo Afisa wa afya dhamana katika bandari ya malindi Ali Hamad Ali alieleza kuwa wanahakikisha abiria wote wanaoingia au kutoka wanapimwa joto la mwili sambamba na kunawa mikono kabla ya kupanda chombo.

“Utaratibu wetu ni kuhakikisha kuwa kila abiria ananawa mikono kabla ya kuingia bandarini lakini pia kupanda vyombo huku tukihakikisha tunawapima joto la mwili na tunaowabaini kuwa na joto kubwa huwaweka chini ya uangalizi kwa uchunguzi zaidi,” alieleza.

Alieleza kuwa toka kuanza kwa utaratibu huo jumla ya watu watano walipatikana wakiwa na joto kali na baada ya uchunguzi Zaidi walibainika kuwa na homa za kawaida na matatizo mengine ya kiafya.

Hivyo aliwataka watu wanaotumia bandari hiyo kuwa tayari kufuata maelekezo wanayoyatoa ili kuepusha madhara yanayotokana na maradhi hayo.

Akizungumza katika kikao hicho, mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Hassan Khatib Hassan alieleza hatua mbali mbali zilizochukuliwa na ofisi yake, wakuu wa wa wilaya na mabaraza ya manispaa na kuhimiza kuendelezwa kwa ushirikiano katika vita hiyo.

“Kuna hatua mbali mbali ambazo tumechukua ambazo zimechangia katika mabadiliko mliyoyashihudia ingawa bado kuna tatizo la usimamizi katika utekelezaji wa maagizo jambo ambalo tunaenda kulifanyia kazi,” alisema Hassan.

Ziara hiyo ambayo ilishirikisha wajumbe wa kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya, wajumbe wa kamati ya kitaifa wajumbe wa kamati ya kitaifa waliwataka viongozi hao kutosita kuomba msaada kwa kamati hiyo ili kusaidia utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa.

About Celebu 6111 Articles
Number 1 Online Kenya/East Africa Music Distributions and Promotion, All Rights Reserved. On DJ Celebu website we offer you some DJ Mixtapes, Gengetone, RnB, Hip Hop, Reggae, Gospel, Bongo Flava, Taarab, Asili, Mp3 Audio Downloads, Mp4 Videos Downloads.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*