Ligi za Soka nchini Ujerumani kurejea mwezi ujao

Bodi inayosimamia ligi za soka za nchini Ujerumani DFL kesho inatarajiwa kufanya mkutano maalum na viongozi wa timu 36 za soka za nchini humo ili kuamua tarehe rasmi ndani ya mwezi ujao ya kurejea kwa ligi zilizosimama kutokana na janga la Corona.

DFL imeazimia kumalizia sehemu iliyosalia ya msimu wa 2019-2020 kuanzia mwezi Mei, huku mamlaka za afya nchini Ujerumani zikipendekeza kuwa mechi zifanyike bila mashabiki iwapo muafaka wa utapatikana kwa ligi hiyo kufanyika mwezi Mei.

Tarehe iliyopendekezwa na DFL kwa ligi hizo kurejea ni 16 na 23 mwezi Mei, na hii ikiwa ni kutokana na mafanikio yaliyopatikana ya udhibiti wa janga la Corona nchini Ujerumani.

Wakati hayo yakiendelea tayari baadhi ya timu zinazoshiriki ligi hiyo zimeanza maandalizi muhimu kwa tofauti tofauti kulingana na maelekezo ya serikali.

About Celebu 6164 Articles
Number 1 Online Kenya/East Africa Music Distributions and Promotion, All Rights Reserved. On DJ Celebu website we offer you some DJ Mixtapes, Gengetone, RnB, Hip Hop, Reggae, Gospel, Bongo Flava, Taarab, Asili, Mp3 Audio Downloads, Mp4 Videos Downloads.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*