Mkutano wa EU kuhusu corona kufanyika leo

Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanajitarisha kwa mkutano mwingine wa kilele unaofanyika leo kutathmini hasara iliyotokana na janga la virusi vya corona kwa chumi za kanda hiyo pamoja na maisha ya watu.

Mkutano huo utakaondeshwa kwa njia ya video unanuwia kuidhinisha mpango kabambe wa kufufua uchumi wakati mataifa ya Ulaya yameanza kuondoa vizuizi vilivyowekwa kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona.

Viongozi 27 wa nchi wanachama wanatakiwa kukubiliana kuhusu hatua za matumizi pamoja kufanya mashauriano juu ya mkakati wa uokozi unaotarajiwa kutangazwa wiki zinazokuja.

 Hata hivyo mkutano wa leo, unaandamwa na kiwingu cha kuporomoka imani miongoni mwa mataifa wanachama juu ya iwapo nchi tajiri za kanda hiyo zitakuwa tayari kubeba jukumu la kuzisaidia kifedha nchi nyingine kujikwamua na athari za kadhia ya corona.

About Celebu 6109 Articles
Number 1 Online Kenya/East Africa Music Distributions and Promotion, All Rights Reserved. On DJ Celebu website we offer you some DJ Mixtapes, Gengetone, RnB, Hip Hop, Reggae, Gospel, Bongo Flava, Taarab, Asili, Mp3 Audio Downloads, Mp4 Videos Downloads.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*