Ozil akataa kupunguza mshahara wake

KIUNGO Mesut Ozil inadaiwa ni miongoni mwa wachezaji watatu ndani ya Arsenal waliyokataa kuchukua mshahara uliyopunguzwa kwa asilimia 12.5. 

Juzi, Jumatatu, Washika Bundika walitangaza kuwa timu ya kwanza ya Ligi Kuu England kupunguza mishahara ya wachezaji kutokana na janga la virusi vya corona. 

Ozil ni mchezaji wa Arsenal anayelipwa mshahara mkubwa wa pauni za Uingereza 350,000 (takribani shilingi bilioni moja) kwa wiki na kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, bado hajashawishika na umuhimu wa mishahara kupunguzwa badala yake akipendekeza ucheleweshwe. 

Inaelezwa kuwa anaweza kuwa tayari kuchukua mshahara pungufu katika siku za usoni lakini anataka kuona madhara kamili ya kiuchumi yanayotokana na virusi vya corona kabla ya kufanya uamuzi. 

Aidha imeripotiwa kuwa yupo tayari kukubali kucheleweshewe kwa zaidi ya asilimia 12.5 ambayo wachezaji wenzake wamechukua. 

Chama cha wachezaji wa kulipwa imewashauri wachezaji dhidi ya kuchukua mshahara pungufu wakati wakala wa Ozil, Dkt. Erkut Sogut hivi karibuni pia alisema wachezaji wasikubali pungufu ya mishahara. 

 “Kucheleweshwa ni wazo zuri lakini sio kukubali kukatwa leo wakati klabu bado zinaweza kutengeneza faida ile ile kama mwaka uliyopita,” alisema. 

“Madhara ya kiuchumi kwenye klabu tunaweza kuona miezi mitatu mpaka sita inayokuja – lakini hatuwezi kuiona leo.” 

Hata hivyo uamuzi wa Ozil haujapokelewa vyema na gwiji wa Manchester United, Gary Neville, akisema ni utetezi dhaifu. 

“Nadhani hayo ndiyo matatizo makubwa unapokuwa na kundi la wachezaji ambao hawapo mrengo moja ndani na nje ya uwanja,” alisema. 

“Nisingependa kuwa moja kati ya wachezaji watatu ambao hawajakubaliana na kundi. Nadhani kuanzia hapo watatengewa kutokana na mambo mengi.” 

Kwa misimu ya hivi karibuni, Ozil amekuwa akisutumiwa kutokana na kupanda na kushuka kwa kiwango chake lakini amekuwa akisifiwa kazi zake za kijamii kusaidia wasiojiweza. 

Mwaka 2014 baada ya kutwaa Kombe la Dunia na timu yake ya taifa ya Ujerumani, kiungo huyo wa zamani wa Real Madrid alitoa fedha zake zote za ushindi kwa hospitali ya watoto nchini Brazil na kwasasa yeye ni balozi wa kituo cha watoto cha Rays of Sunshine. 

About Celebu 6159 Articles
Number 1 Online Kenya/East Africa Music Distributions and Promotion, All Rights Reserved. On DJ Celebu website we offer you some DJ Mixtapes, Gengetone, RnB, Hip Hop, Reggae, Gospel, Bongo Flava, Taarab, Asili, Mp3 Audio Downloads, Mp4 Videos Downloads.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*