TAROTWU walaani taarifa ya mgomo wa madereva

Chama cha Wafanyakazi wa Usafirishaji kwa njia ya Barabara Tanzania (TAROTWU) kimewataka madereva wote nchini kupuuza taarifa ya kuwepo kwa mgomo kwa madereva ifikapo Aprili 30 mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi Habari Katibu Mkuu wa Chama hicho Salum Abdallah amesema kuwa baadhi ya vyama viliitisha mgomo huo ambao kwao ni batili.

Amesema Serikali iliitisha kikao cha dharura kwa Vyama vinavyohusika katika sekta ya usafirishaji kilichofabyika Jijini Dar es Salaam hivi karibuni na kuzungumza masuala mbalimbali na kusema masuala yao yanashughulikiwa

Abdallah amewataka madereva wote nchini wafuate sheria zilizowekwa hivyo kitendo kilichofanywa na baadhi ya vyama kuhitisha mgomo ni kukiuka sheria na utaratibu.

“Tunawaomba wanachama wetu hasa madereva wafuate sheria wasigome, Chama cha TAROTWU hatuna mpango huo wa kugomesha madereva na hata hivyo Vyama vingine wamesema hawana mpango huo”. Amesema Abdallah.

Aidha Bw.Abdallah amesema kuwa katika kikao walichokaa hivu karibuni Vyama ambavyo vilikiuka sheria kwa kuwataka madereva Kugoma navyo vimekiri kufanya makosa na vitaweka wazi kusitisha mpango huo.

“Kitendo hiki tunakilaani kama Chama na hivyo tunaiomba Serikali ichukue hatua madhubuti kwa watu ambao sasa hivi wameingia kwenye utaratibu wa kuleta migongano na mitafaruku katika sekta ya usafirishaji bila sababu ya msingi”. Amesema Abdallah.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama hicho Bw.Shukuru Mlawa amesema kuwa katika kikao cha dharura walichokaa na Serikali kilihusisha vyama vyote vinne vinavyohusika katika sekta ya Usafirishaji vyama hivyo ni pamoja na TAROTWU,COTWU,CHAWAMATA na TADWU.

Pamoja na hayo Mlawa amesema kuwa wao wanaamini serikali ni sikivu hivyo itaendelea kusikiliza changamoto zinazowakabili madereva hapa nchini na kutatuliwa changamoto zao.

Amesema serikali iko katika mapambano ya ugonjwa wa Virusi vya Corona hivyo masuala mengine hayana nafasi katika kipindi hiki.

About Celebu 6076 Articles
Number 1 Online Kenya/East Africa Music Distributions and Promotion, All Rights Reserved. On DJ Celebu website we offer you some DJ Mixtapes, Gengetone, RnB, Hip Hop, Reggae, Gospel, Bongo Flava, Taarab, Asili, Mp3 Audio Downloads, Mp4 Videos Downloads.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*