Swahili News

Ujerumani yapoteza udhibiti wa kupungua kwa maambukizo ya virusi vya corona

on

[ad_1]

Idadi ya maambukizo mapya ya virusi vya corona inayotangazwa kila siku nchini Ujerumani sasa inapanda, maafisa wa udhibiti wa magonjwa wamesema katika ripoti yao mpya, ikiwa ni pigo kwa nchi hiyo wakati ikichukua hatua taratibu kuondoa vizuwizi vyenye lengo la kudhibiti virusi hivyo.

 Ripoti kutoka katika taasisi ya serikali ya Robert Koch iliyotolewa jana jioni inaonesha ongezeko la idadi, ambapo idadi ya mtu ambaye anaambukiza wengine virusi hivyo imeongezeka kwa mtu mmoja.

Tarakimu hizo zilikuwa katika siku za karibuni zimefikia 0.9, ambapo maafisa wamesisitiza kuwa sasa Ujerumani inarudi nyuma na kuwa na kuwa na uwezekano wa kusambaa tena kwa ugonjwa wa COVID-19 iwapo maambukizo yatafikia zaidi ya mtu mmoja.

Maduka mengi makubwa na ya kati yamefunguliwa nchini Ujerumani wiki iliyopita na majimbo mengi yanatarajia kuruhusu shule kufunguliwa tena kuanzia Mei 4, lakini takwimu hizi mpya ni pigo kwa juhudi za kurejesha tena maisha ya kawaida.

[ad_2]

About Richard Wanyonyi

Richard Wanyonyi

Leave a Reply