Wamarekani milioni 26 waomba msaada wa ukosefu wa ajira Marekani tangu mripuko wa corona

Zaidi ya watu milioni 4.4 walioachishwa kazi nchini Marekani wametoa maombi ya kupatiwa mafao ya wasio na ajira wiki iliyopita, wakati ambapo upunguzaji wa ajira ukiongezeka katika uchumi ambao umeendela kufungwa kutokoana na janga la virusi vya corona.

Karibu watu milioni 26 wamejiandikisha kutokuwa na ajira tangu mripuko wa corona ulipoanza kuwalaazimisha mamilioni ya waajiri kufunga biashara zao.

Karibu katika kila wafanyakazi sita nchini Marekani amepoteza kazi yake katika muda wa wiki tano zilizopita, katika hali mbaya zaidi ya usitishaji wa ajira katika historia ya taifa hilo.

Wachumi wamekadiria kuwa kiwango cha ukosefu wa ajira kwa mwezi Aprili kinaweza kufikia hadi asilimia 20.

Usitishaji huo wa ajira umeutumbukiza uchumi wa Marekani katika mzozo mkubwa zaidi wa kiuchumi tangu mdororo mkubwa wa miaka ya 1930.

Baadhi ya wachumi wanasema uzalishaji nchini humo unaweza kushuka kwa mara ya mbili ya kiwango kilichoshuhudiwa wakati wa mporomoko mkubwa uliomalizika mwaka 2009.

About Celebu 6159 Articles
Number 1 Online Kenya/East Africa Music Distributions and Promotion, All Rights Reserved. On DJ Celebu website we offer you some DJ Mixtapes, Gengetone, RnB, Hip Hop, Reggae, Gospel, Bongo Flava, Taarab, Asili, Mp3 Audio Downloads, Mp4 Videos Downloads.

Be the first to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.


*