Swahili News

WHO yaonya kuhusu kuvurugika kwa njia za kusambaza vifaa

on

[ad_1]

Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO, limetoa wito wa kusaidiwa ili kusafirisha vifaa vya uchunguzi na vya kujikinga katika maeneo ambako ugonjwa wa COVID-19 unasambaa, hususan Amerika ya Kusini.

Paul Molinaro, mkuu wa operesheni na usafirishaji wa WHO, amesema usafirishaji duniani wa chanjo umevurugika mwezi Aprili na iwapo hali hii itaendelea hadi Mei kutakuwa na upungufu katika utoaji wa chanjo na kampeni dhidi ya kuzuka kwa magonjwa mengine.

Ameongeza kuwa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Chakula, WFP, umeripoti kuvurugika kwa mara ya kwanza usambazaji wa chakula ambao unaweza kuathiri zaidi juhudi za kupambana na mripuko wa virusi vya Corona.

Safari za ndege na za baharini zimeathirika sana kutokana na marufuku iliyowekwa na mataifa kadhaa katika kukabiliana na kusambaa kwa virusi hivyo, ingawa kimsingi usafirishaji bidhaa na vifaa vya matibabu ulikusudiwa usiguswe na marufuku hizo.

[ad_2]

About Richard Wanyonyi

Richard Wanyonyi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *